Katibu Mkuu Wa Uchukuzi Atembelea Banda La Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege Tanzania(TAA)

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usalama TAA Bw, Bakari Mwalwisi ( mwenye tshirt nyekundu) juu ya vifaa vinavyozuiwa kuingia katika ndege wakati wa safari alipotembelea  katika banda la Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho  (mwenye suti ya kijivu) akisaini katika kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akifurahia jambo kutoka kwenye kipeperushi  mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania katika Viwanja vya maonesho ya nanenane Nyakabindi Mkoani Simiyu .
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano alipotembelea mabanda ya Taasisi hizo katika maonesho ya sikukuu ya Wakulima nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Post a Comment

Previous Post Next Post