OLWERO: VIPIMO SAHIHI NI MSINGI WA MAAMUZI YA MAENDELEO


 Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) umeeleza kuwa matumizi ya vipimo sahihi yana mchango mkubwa katika kupanga sera na kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo ya kiuchumi nchini.

Akizungumza na watumishi wa wakala huo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka WMA, Francis Olwero, amesema  takwimu zinazotokana na vipimo sahihi husaidia serikali kupanga sera zenye tija katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, viwanda na huduma  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo huadhimishwa Mei 20 kila mwaka.

Olwero amesema  matumizi ya vipimo visivyo sahihi yanaweza kuathiri ukusanyaji wa taarifa muhimu za uzalishaji na biashara, hali inayoweza kusababisha upangaji usio sahihi wa mipango ya maendeleo na matumizi mabaya ya rasilimali.

“WMA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia mizani na vipimo vilivyothibitishwa ili kujenga uchumi wenye ushindani, uwazi na unaolinda maslahi ya walaji pamoja na wafanyabiashara.”amesema Bw.Olwero

  \       



Post a Comment

Previous Post Next Post