TFRA Yaimarisha Utaalamu wa Watumishi Kupitia Mafunzo

Mwandishi Wetu,

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeendelea kuwekeza katika kukuza ujuzi wa watumishi wake baada ya maafisa wake kuhitimisha mafunzo ya itifaki na mahusiano ya umma yaliyofanyika kuanzia Mei 4–8, 2026 katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

Mafunzo hayo yalitolewa kwa maafisa watatu ikiwa ni pamoja na Nuru Mwasampeta, Beatrice Bazazi na Zainab Mzee yatasaidia katika kuongeza ufanisi katika masuala ya mawasiliano ya taasisi, kuboresha huduma kwa umma na kuimarisha utendaji wa majukumu ya kila siku. 

Washiriki wamepata ujuzi katika masuala ya Mawasiliano ya kimkakati,

Uhusiano na vyombo vya habari, Maadili ya utumishi wa umma, Utunzaji wa taswira ya taasisi na namna bora ya kudumisha mashirikiano baina ya wadau wa taasisi na kampuni wanazozifanyia kazi.

Afisa Uhusiano, Nuru Mwasampeta, ameishukuru Menejimenti ya TFRA kwa kutoa nafasi ya mafunzo hayo, akieleza kuwa yameongeza tija katika kazi na maisha binafsi.

Kwa upande wake, Afisa Biashara, Beatrice Bazazi, amesema mafunzo hayo yataimarisha uhusiano kati ya taasisi na wadau pamoja na kuongeza ufanisi kazini.


Post a Comment

Previous Post Next Post