
Bungeni Dodoma,
Serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii imeainisha vipaumbele tisa vya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2026/2027, vikiwa na lengo la kuimarisha sekta ya utalii, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za taifa.
Akiwasilisha bajeti ya wizara hio waziri Dkt. Ashatu Kijaji Mei 15, 2026, , amesema Kuwa Kati ya vipaumbele hivyo ni kuimarisha utangazaji wa utalii ndani na nje ya nchi kwa kutumia mikakati mahsusi ikiwemo masoko ya Mashariki ya Mbali na Mashariki ya Kati.
Pia, amebainisha Kuwa serikali itaendelea kuboresha mazao ya utalii ya kimkakati ikiwemo utalii wa meli, mikutano na matukio (MICE) pamoja na kutambua na kusajili mazao mapya ya utalii.
Aidha, vipaumbele hivyo vinajumuisha kuimarisha miundombinu wezeshi katika maeneo ya utalii na hifadhi, ikiwemo barabara, viwanja vya ndege, mawasiliano na huduma za kijamii.
Katika hatua nyingine, serikali imeeleza kuimarisha ulinzi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori, misitu, nyuki na malikale.
Vilevile, kuimarisha uzalishaji, uongezaji thamani na masoko ya mazao ya misitu na nyuki ni miongoni mwa vipaumbele vilivyotajwa katika bajeti hiyo.
Bajeti hio pia imebainisha nafasi ya Hifadhi za Taifa (TANZANIA NATIONAL PARKS) katika utekelezaji wa majukumu ya sekta ya maliasili na utalii.