
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Palamagamba J.A. Kabudi wakati wa kikao cha 7 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 13 Aprili, 2026 Jijini Dodoma.
Mkutano huo wa Tatu wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma ni Mahsusi kwa ajili ya kujadili Utekelezaji wa Bajeti za Wizara zote kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.