WANAHABARI WAHAMASISHWA KUTUPIA JICHO KILIMO IKOLOJIA


 NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

WITO umetolewa kwa waandishi wa habari nchini kuandika habari za Kilimo Ikolojia ili kuhamasisha wakulima kubadilika na kuingia katika kilicho hicho ambacho kimekuwa na manufaa  makubwa katika afya ya bindamu na kulinda mazingira ya kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za Kilimo Ikolojia iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi wa taasisi ya Iles De Paix In Tanzania (IDP), Asiye Buberwa ameweka wazi kwamba chakula ni kisababishi kikubwa cha afya mbaya kwa binadamu.

Amefafanua kwamba waandishi wa habari wakijikita zaidi kuandika habari za Kilimo Ikolojia itasaidia kwa asilimia kubwa wananchi kutumia mazao yanayokuzwa kwa kutumia mbinu za Kilimo Ikolojia.

“Leo tumekutana na wanahabari hapa Arusha, lengo ni kuhakikisha habari kuhusu mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia Kilimo Ikolojia inasambaa na kuungwa mkono kila kona ya Tanzania na wakulima kugeukia kilimo hiki na pia kupitia nyinyi changamoto zitaibuliwa kutokakwa  wakulima ili kupata mafanikio stahiki,” amesema.  

Pia ametanabaisha kwamba tangu shirika hilo lianze kufanya shughuli hapa Tanzania mwaka 2015 wanafanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa kitazania ikiwemo Chuo cha Kilimo Morogoro (SUA), Chuo Cha Nelson Mandela cha jijini Arusha na lengo kubwa likiwa hata wakiondoka shughuli za Kilimo Ikolojia ziendedee.

Amesema wadau wengine ambao wanashirikiana nao ni Mtandao wa Vikundi vya Wakulima mkoani Arusha (MVIWAARUSHA), Shirikisho  la Vyama Wakulima Wadogo Tanzania (SHIWAKUTA) pamoja na taasisi ya Research Community and Organization Development Associates (RECODA).

mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post