TFRA yaendelea kuimarisha ushirikiano na wazalishaji wa ndani wa mbolea


 Mwandishi Wetu,

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetembelea mkulima anayelima mbogamboga katika Mtaa wa Mpiji Muheza, Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, kwa lengo la kujionea ufanisi wa mbolea iliyozalishwa na kijana wa Kitanzania ya Mtetezi Halisi.

Akizungumza shambani hapo leo tarehe 28 Februari,2026  afisa udhibiti ubora mwandamizi kutoka TFRA Stephano Mfugale amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi, kuhakikisha kuwa uzalishaji wa ndani wa mbolea na visaidizi vyake unaongezeka.

 Mfugale ameongeza kuwa TFRA inaendelea kuzitangaza fursa za uwekezaji katika tasnia ya mbolea na kuwapongeza wazalishaji wa Mtetezi Halisi kwa kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni  ya Mtetezi Halisi  inayozalisha mbolea za kimiminika Raymond Simya, ameishukuru TFRA kwa ushirikiano walioupata hadi kufanikisha usajili wa mbolea hiyo. 

Simya amesema,hatua hiyo imefungua fursa kwa wazalishaji wa ndani kushiriki kikamilifu katika tasnia ya mbolea.

Kwa upande wake, mkulima anayetumia mbolea za Mtetezi Halisi Rehema  Bombo amesema tangu aanze kutumia mbolea hiyo ameshuhudia mabadiliko chanya katika ukuaji wa mazao yake.

TFRA inatekeleza majukumu yake kwa kuwafikia wadau wakiwemo wazalishaji wa ndani wa mbolea na wafanyabiashara na wakulima ili kuhakikisha tasnia ya mbolea inaimarika zaidi.



Post a Comment

Previous Post Next Post