SIKU 100 ZA RAIS SAMIA MADARAKANI ZAIMARISHA SOKO LA AJIRA ZA NDANI NA KIMATAIFA.


 Mwandishi Wetu Dar-es-salaam,

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mhe. Prof. Adolph Mkenda ameyasema hayo,  wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Shirikishi wa Vyuo Vikuu na Viwanda uliozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 9 Februari 2026 , JNICC,  Mtaa wa Shabani Robert,  Wilayani Ilala CBD - Jijini Dar es salaam. 

" Mhe. Makamu wa Rais itakumbukwa tarehe 28 Februari 2025 wakati Mheshimiwa Rais akifungua kampeni za Uchaguzi  Mkuu kwa niaba ya Taifa na  Chama Cha Mapinduzi alitoa ahadi hiyo wakati akiapishwa kuwa Serikali itaandaa na kuzindua mpango wa Kitaifa wa pamoja kati ya Vyuo na Waaajiri Nchini" alisisitiza Prof. Mkenda.  

Prof mkenda amesema Mpango huu umekamilika kabla ya Siku 100 za Ahadi za Mheshimiwa Rais hazijaisha tayari umezinduliwa na kuongeza kuwa mpango huo ni Shirikishi kwa kuwa umeshirikisha Taasisi na wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu na Viwanda kuimarisha Ujuzi , Stadi na Uwezo wa wahitimu kuajirikia katika  Soko la Ajira za Ndani na Nje ya Nchi. 

" Mafanikio ya Mpango huu ni baadhi ya wahitimu kuajiriwa na Vyombo vya Habari  kwenye Mataifa kama Namibia, Guinea- Conakry. Mauritiania, Congo na Ghana. Ambapo wahitimu wameonesha wanasoko kubwa la Ajira la Ndani na Nje ya nchi.  Na hili pia mhe rais aliliweka kama sehemu ya Ahadi yake leo na yanatimia. Naomba nikushukuru sana Makamu wa Rais kwa kukubali kuja hapa leo na kuonesha umuhimu wa Uzinduzi wa mpango huu " alisisitiza Prof. Mkenda. 

.Aidha, Prof mkenda alipongeza waandaaji, Viongozi wa chama, Viongozi wa Dini na utayari wa  Seikali kupokea na kupongeza Juhudi za maksudi zilizochukuliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutimiza Ahadi ya Mhe. Rais na kupongeza utolewaji wa hali na mali wa Wadau tofauti kuwezesha Sekta ya Elimu kusimamia utekelezaji wa Mpango huo kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 (Toleo 2023) kuzalisha rasilimaliwatu mahiri yenye ujuzi na uwezo wa kuajirika Soko la Ajira za Ndani na Nje ya Nchi.

#CostechTanzania 


Post a Comment

Previous Post Next Post