Mwandishi Wetu Dar- es- salaam,
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo 2023) inabainisha wazi kuwa ushirikiano wa Mafunzo kati ya Vyuo na wazalishaji si hiari bali ni wajibu wa kimfumo ili kuhakikisha stadi zinazozalishwa zinawiana na mahitaji halisi ya Soko la Ajira na uchocheaji wa ukuaji wa kiuchumi.
Mhe. Wanu ameyasema hayo tarehe 9 Februari 2026 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya Vyuo na Viwanda uliofanyika Ukumbi wa JNICC, uliopo mtaa wa Shabani Robert, Wilayani Ilala - Jijini Dar es salaam.
" Mheshimiwa Mgeni rasmi kwa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wizara imeandaa Mpango wa pamoja wa Ushirikiano kati ya Waajiri na Vyuo " alisema Mhe. Wanu
Aidha, Mhe. Wanu amebainisha kuwa Mpaka sasa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekwisha anzisha Kamati 33 za Ushauri wa Kitaalamu na kitasnia yaani " Industrial Advisory Committee " na kuingia kwa mikataba ya hati za Makubaliano (MOU) mbalimbali ikiwemo mikataba 50 ya VETA na Viwanda .
" Mikataba zaidi ya 250 katika Taasisi za Elimu ya Juu na Viwanda, na mikataba 76 ya Vyuo vya Ufundi na Viwanda. Mhe. Mgeni rasmi ninayofuraha kuwatambua kipekee baadhi ya wadau muhimu walioleta mafanikio makubwa kwa wahitimu wetu kupitia mikataba ya Ushirikiano na kutoa fursa ya ajira kwa vitendo" alisisitiza Mhe. Wanu
Vilevile, Mhe Wanu ametambua na kupongeza jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali kusaidia Wizara kutekeleza ahadi za Mhe Rais ikiwemo sekta binafsi inayojumuisha Alminium Emirates na Chuo cha VETA kuwezesha wanafunzi na wakufunzi utengenezaji wa bidhaa za Alminium na chuma na kuandaa mtaala wa kozi za muda mrefu za Alminium, glass na metal works. PILI, SATAN Corp. Ltd wakishirikiana na VETA kutoa mafunzo kwa vitendo ya uunganishwaji wa Mabasi na Malori na Asilimia 80 ya wafanyakazi wao ni wahitimu wa VETA.
" Tunao pia Simba Supply Chain Service na Chuo cha NIT wanashirikiana pamoja kuandaa na kuendeleza ujuzi wa wanafunzi na wakufunzi ili kuongeza thamani ya mnyororo wa ugavi, usafiriishaji, uhandishi na TEHAMA kupitia mafunzo kwa vitendo kazini, ajira na ujenzi wa uwezo wa matengenezo kazini. Vilevile precision Air wanashirikiana programu za mafunzo kwa vitendo , kujitolea kazini 'internship ' na ajira kwa wahitimu. Pamoja na Anna fashion na VETA utengenezaji wa mavazi na Kilimanjaro international leather industry co. Ltd wanasirikiana na DIT kupitia programu za usindikaji wa ngozi na Teknolojia za uzalishaji bidhaa za ngozi" alihitimisha
Amehitimisha kwa kutambua ushirikiano wa Sekta Binafsi ya Kagera Sugar , Magic Builders na wengine wengi wanashirikisha katika kutoa ajira na kukuza michango hivyo Serikali inatambua michango yao na inapongeza kwa dhati jitahada zao za makusudi.




