MOI KUFANYA UPASUAJI WA SARATANI YA UBONGO

 

KWA Mara ya kwanza Taasisi ya Tiba ya Ubongo na Mifupa Muhimbili(MOI) inatarajia kufanya upasuaji wa kisasa wa kutoa uvimbe kwa saratani katika ubongo kwa kutumia rangi maalum kwa watu 10.

Akizungumza Katika Mkutano wa tano wa Kimataifa wa wataalamu wa Uti wa mgongo,mishipa ya fahamu na Ubongo unaofanyika leo jijini Dar es Salaam ukihusisha madaktari Bingwa kutoka Chuo kikuu cha Colorado cha nchini Marekani ,Daktari Bingwa wa Ubongo,Mishipa ya fahamu na uti wa mgongo  kutoa MOI, Dk. Nicephorous Rutabasibwa amesema pia watafanya na huduma ya utengamao.

“Kuna dawa tunaitumia na ukiitumia ule uvimbe unajionesha moja kwa moja  inamwezesha daktari kuweza kutoa uvimbe wote bila kubakiza chochote ,Ndo teknolojia mpya ambayo tunaifanya tutatumia microscop na ultrasound na hizo dawa tulizoletewa.

Ameongeza “Kwa kutumia hiyo teknolojia kwasababu tayari tuna wataalamu ambao wamekuja kutufundisha tunategemea kufanyia wagonjwa ambao tumeshawaandaa kwaaajili hiyo kwasababu teknolojia tutabaki nao tutakuwa tunafanya wenyewe.

Akifungua Mkutano huo Mkurugezni Mtendaji wa MOI Balozi Dk Mpoki Ulisubisya amesema pamoja na kubadilishana Mawazo kupitia mada mbalimbali ambazo zinatolewa kuna aina nyingine ya mafunzo yatakayokuwa yanatolewa  kwa wataalamu ambao wanaibukia kutoa  kutoa huduma kwa wagonjwa ambao wanakuwa wamefashafanyiwa matibabu namna ya kuwafatilia.

“Hapa tutakuwa na wauguzi watafundishwa namna ya kuhudumia wagonjwa mahututi ambao wamefanyiwa  upasuaji katika  mfumo wa fahamu tutakuwa na wataalamu wa utengemao kwa mara ya kwanza MOI inatoa mafunzo kwa madaktari ambao watakuwa wanasimamia kazi ya utengamao kwa wagonjwa watakaokuwa wanahitaji,”amesema.

Amesema wanafanya mkakati huo kutokana na kutarajia kutoa huduma ya utengemao kwani  kuna sehemu maalum ya utengamao ambayo  inajengwa kule Mbweni “Kutakuwa na mkusanyiko wa kufundisha hawa wataalamu baada ya mada kuwasilishwa kwa  vitendo wataalamu watafanya upasuaji  kuna zile  njia za matundu,Kuna watu wametoka nchi mbalimbali za Afrika kuja kupata ufahamu ,tumekuwa na mahusanao haya  na Chuo kikuu cha Colorado kutoka Marekani wamejua na mzigo wa vitu vya kutumia kwaajili ya upasuajia katika maeneo  ya mfumo wa fahamu,”amesema Dk Mpoki.

Kwa upande wake Prof  Ryan Ormond kutoka chuo Kikuu cha Colorado Marekani ambaye pia ni Msimamzi mkuu wa kimataifa wa mkutano huo amesema  mkutano mada nyingi ikiwa ni pamoja  na maendeleo ya kisayansi ya hivi karibu katika udhibiti wamaradhi mbalimbali ya uvimbe wa ubongo na uti wa mgongo .

“Tunafanya kwa vitendao katika vyumba vya upasuaji itafanyika teknolojia muhimu zitatumika tutafanya usimamizi wa matibabu ya kupunguza vichwa vikubwa kwa Watoto,matibabu  ya wagonjwa mahututi wa neva ,elimu ya uuguzi na ukarabati wa neva,”amesisitiza.

Post a Comment

Previous Post Next Post