TFRA yawahakikishia wakulima wa Songwe upatikanaji wa mbolea pindi msimu utakapoanza

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent, amewahakikishia wakulima wa mkoa wa Songwe upatikanaji wa mbolea kwa msimu ujao wa kilimo.

Akizungumza leo tarehe 25 Septemba 2025 katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabili Makame, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Laurent amesema ziara yake mkoani humo inalengo la kusalimia, kujitambulisha na kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea mkoani humo. 

Kwa upande wake Mhe. Makame ameahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Serikali ya Mkoa wa Songwe katika kuhakikisha tasnia ya mbolea inasimamiwa ipasavyo. 

Aidha, amebainisha umuhimu wa Mkoa huo kwa Taifa ikiwa ni mkoa wa pili kwenye matumizi makubwa ya mbolea na ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini




Post a Comment

Previous Post Next Post