BURAH: NIKIWA DIWANI KATA KILAWANI WANANCHI WATANUFAIKA NA UWEPO WA VIWANDA


 NA MWANDISHI WETU

WAKAZI wa Kata ya Kilawani, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wanatarajiwa kunufuika na ajira za viwandani ikiwa mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Burah atapata ridhaa ya kuwa diwani katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“Kata yetu imefanikiwa kuzungukwa na viwanda vingi lakini asilimia 90 ya wanaofanyakazi katika viwanda hivyo wanatoka nje ya kata hii, hivyo nikiingia madarakani nitatumia ushawishi wangu kuzungumza na viongozi wa viwanda hivyo kupitisha nafasi za ajira katika ofisi ya diwani ili iwe rahisi vijana wetu kupata ajira katika hivyo,zitakazowaondoa katika changamoto ya ukosefu wa ajira ” amesema.

Burah ameweka wazi hayo leo, Agosti 31, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika kata hiyo kutaka kujua mikakati yake ikiwa atafanikiwa kuwa diwani katika Uchaguzi Mkuu ujao na akaongeza kwamba vipambele vingine ambavyo atavisimamia ni kuhakikisha akina mama, makundi maalumu wanajikwamua kiuchumi kupitia mikopo nafuu.

Amesema ni kipindi kirefu kumekuwa na malalamiko ya makundi hayo kutopata mikopo inayoweza  kuwakwamua kiuchumi kutokana na kuwekwa masharti magumu na hata ile ya asilimia 10 imekuwa changamoto nyingi hadi kumfikia muhitaji.

Pia amesema jambo lingine ambalo atakwenda kulisimamia ikiwa atapata ridhaa ya wananchi kuongoza kata hiyo na kutekeleza ilani Ilani ya CCM ipasavyo ni kuhakikisha sifuri kwa matokea ya kitado cha nne zinaondoka ili kutoa nafasi kwa wahitimu kuendelea na masomo ya juu.

“Naumia sana kuona kata hii inakuwa ya mwisho katika matiokeo ya kidato cha nne, sijajua tatizo liko kwa walimu au wanafunzi ama wazazi pindi nitakapofanikiwa kuingia madarakani nitafanya tafiti ya kutosha ili kupata kiini ya kwanini sifuri zinakuwa nyingi ili kuzipunguza kwa asilimia kubwa.

 “Hivyo naomba wananchi waniunge mkono kwa kunipigia kura kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu ujao wakianza kwa nafasi ya udiwani, ubunge na urais tupate kura za kishindo ili changamoto zilizopo katika kati yetu, tuweze kuzitatua kwa kauli moja, naamini nikishirikiana na wezangu hakuna kitakachoshindikana,” amesema.



Post a Comment

Previous Post Next Post