Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James.
Mhe. Aweso katika kikao hicho katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Iringa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Mwajuma Waziri.
Kikao kimehusu utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 ambao unatekelezwa wilayani Mafinga.
Waziri Aweso amemhakikishia Mkuu wa Mkoa na wananchi kuwa Wizara ya Maji inafuatilia kwa karibu kazi hiyo ili kuhakikisha kazi inakamilika na kufikisha huduma ya uhakika ya majisafi na salama kwa wananchi.