ZIMEBAKI SIKU SITA KUELEKEA UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 IRINGA

 Mwandishi Wetu,

Mkoa wa Iringa unajiandaa kupokea wanamichezo kutoka mikoa mbalimbali nchini, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa shule za Msingi na Sekondari yanayotarajia kuanza tarehe 7 Juni 2025.

Mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwaka yanaratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita tangu 2022, mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA yalifanyika Mkoani Tabora, na mwaka huu yanafanyika Mkoani Iringa yakitarajiwa kuhusisha wanamichezo zaidi ya 7,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.



Post a Comment

Previous Post Next Post