VIJANA WA TK MOVEMENT ENDELEENI KUMSEMEA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA MAENDELEO ALIYOFANYA NCHINI BILA WOGA "HAPI"

Mwandishi Wetu,

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ally Hapi (MNEC), amewataka vijana wa TK MOVEMENT kote nchini kusimama kidete na kumsemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, bila woga wowote, akisisitiza kuwa kazi kubwa aliyoifanya inaonekana kwa macho.

Hapi amesema hayo mbele ya vijana zaidi ya 1,500 kutoka mikoa yote nchini, waliokusanyika jijini Dodoma kwa ajili ya semina ya kitaifa ya viongozi wa mikoa na wilaya, kuelekea Uchaguzi Mkuu. Semina hiyo ya siku mbili inalenga kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo muhimu.

“Jukumu la kumsemea Rais Samia liko mikononi mwa vijana na kila Mtanzania mpenda maendeleo alichokifanya ni kikubwa mno, na kinahitaji kutangazwa,” amesema Hapi.


Imetolewa na Idara ya Oganaizesheni ya Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa



Post a Comment

Previous Post Next Post