NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania.
Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Asao Keiichiro (Kei).
Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema mashirikano haya yataongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza katika miradi ya biashara ya Kaboni itakayoibuliwa nchini.
.jpg)