Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw. Joel Laurent (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Indorama Group ya nchini Nigeria baada ya kikao kilichojqdili fursa za uwekezaji kwenye tasnia ya mbolea nchini, jana tarehe 22 Aprili 2025Jijini Dar Es Salaam.
Indorama wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha mbolea ya Urea Tanzania ili kuimarisha upatikanaji wa mbolea ndani na katika ukanda wa Afrika Mashariki."
