SERIKALI imedhamiria kujenga misingi shindani na endelevu yenye ubora wa utoaji wa huduma wenye kuwezesha biashara nchini kwa kuzingatia jiografia na rasilimali watu kwa kupitia sera mikakati na mipango shindani na shirikishi.
Ameyasema hayo jana Desemba 6, 2024 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdalah wakati wa hafla fupi ya kupokea Cheti cha umahiri wa kutoa huduma ya Ithibati Ubora na bidhaa kutoka SADCAS iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Ithibati za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCAS) Bi. Eve Christine Gadzikwa amesema kabla ya Cheti hicho cha Umahiri katika Ithibati Ubora,TBS walishapatiwa cheti cha Umahiri katika huduma za Maabara pamoja na cheti katika mifumo ya usimamizi hivyo Shirika hilo linapiga hatua kubwa kwenye Viwango vya ubora.
Amesema ili kuwa na misingi ya ushindani katika soko la ndani na nje na kuwa na ubora wa Kimataifa na kuweza kushindana sokoni ni lazima kuwa na Mamlaka inayohusika na Viwango yenye mifumo inayoatambulika na kuaminika kimataifa kupitia viwango vya kimataifa na hivyo Serikali inatenga bajeti kila mwaka kuwezesha TBS kuboresha mifumo yake ya udhibiti na ubora.
Aidha amesema cheti hicho kwa TBS ni kuthibitisha na kutafsiri maono na miongozo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan juu ya kuingia kwenye masoko ya kimataifa kwa kuwa na bidhaa bora kwani huo ni uthibitisho kuwa bidhaa inayothibitishwa na TBS inaweza kuuzwa kwenye masoko ya Kimataifa hivyo ni fursa kwa Wafanyabiashara na Wazalishaji kutumia Shirika hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, amesema maabara zote tisa za TBS zimeishathibitishwa mifumo na zina Ithibati.
"Lakini pia tumepata Ithibiti ya umahiri katika mifumo ya usimamizi wa viwango kimataifa na TBS inatoa huduma hiyo hapa nchini na mifumo hiyo tayari viwanda na taasisi mbalimbali zimeishathibitishwa," amesema Dkt. Katunzi.
Aidha, Dkt. Katunzi amesema kutokana na kuhimarika kwa uhuduma za shirika, mifumo yake ya udhibiti wa ubora imekuwa ikipokea maombi ya viwanda kutoka nje ili kuweza kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.
Amesema hadi sasa wana takribani bidhaa 87 zinazozalishwa huko duniani ambazo zimethibitishwa ubora wake na TBS na kuweza kutumia nembo ya shirika ya ubora ili bidhaa zake ziweze kutumika hapa nchini.