NA MWANDISHI WETU
CHUO cha Ufundi Stadi cha Furahika, ambacho kipo, Illa Dar es Salaam kimeanzisha kozi mpya ya kuwafundisha wasichana kutoa huduma kwenye mabasi na daladala ukondakta.
KAIMU Mkuu wa Chuo, hicho Dkt David Msuya, amebainisha hayo Desemba 5, 2024 na kufafanua kuwa kozi hiyo inatolewa bure ili kutoa nafasi kwa wasichana kujitojeza kwa wingi.
Dkt Msuya ameongeza kuwa kozi wataifundisha kwa siku 10 na baada ya hapo wahitimu watapatiwa vyeti vya Veta vitakavyowasaidia kuaminika kwenye utafutaji wa kazi ambayo kwa sasa inavutia wasichana wengi.
"Niwaombe wasichana waje Kwa wingi kusoma huu, ili kupata uchuzi wa kutoa huduma kwenye mabasi na zaidi tunalenga mabasi ya mikoani ingawa hata wanaitaka kufanya kazi kwenye daladala nao tunawakarisha.
Lengo letu ni kuwafanya kuwa na weredi wanapokuwa wanatimiza majukumu yao na waachane na kufanya kazi hiyo kwa mazoea jambo litakalowasaidia kupandisha thamani yao, amesama.
Pia ameongeza kuwa wanapokea wasichana kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo, Songea, Mbeya, Njombe ,Mwanza, Shinyanga, Kahama, Geita, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Manyara na Arusha.
"Nawaomba waje kwenye Chuo Cha Furahika ambacho kipo chini ya Veta wapate mafunzo kuhusu njia bora ya kufuata wakati wakitoa huduma ya ukondakta kwenye mabasi," amesema.
"Fani hii mwanafunzi anasoma siku 10 tu, kisha tutampatia cheti cha Veta...ni bure kabisa. Hivyo tunawakaribisha watu wote wanaotaka kujifunza, lengo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ili watu waweze kujiajiri na kuajiriwa," amesema na kuongeza kuwa:
Serikali haiwezi kukuletea vitu nyumbani, kuna vitu lazima sisi wenyewe tupambane kuhakikisha Tanzania ya mama Samia inawezekana kupitia Kampuni zetu na ajira zinapatikana.
"Na ajira zipo wafanyabiashara wanatoa ajira, kampuni binafsi zinatoa ajira. Hivyo waje Furahika kusoma kozi mbalimbali tunazotoa bure kabisa," amesisisitiza.
"Kozi hii ni mpya, kwa wasichana wote, warembo wasikae nyumbani waje wasome na uzuri wa kozi hii hata wa darasa la saba anasoma kwasababu anachojifunza ni customer care kwa mteja na vile vitu ambavyo vinamuhitaji ndani ya gari,".
Amesema kuwa dirisha la usajili limefunguliwa hivyo wanaweza kujiunga kupitia mfumo au kufika chuoni hapo.
Ameongeza kuwa, wanaamini katika kujifunza masomo mbalimbali ya Veta ni njia pekee ya kufanya kijana aondoke kwenye mawazo mabaya.
"Kwahiyo tunaomba wazazi wasiwaache watoto, wawalete waje kujifunza kozi mbalimbali tunazotoa. lakini kimsingi tunaamini Tanzania ya Mama Samia tunahitaji vijana wenye ujuzi ili kwenda na kasi ya soko la ajira.
"Kusoma tu chuo haitoshi, kuna watu Wana degree, PhD lakini anatembea tu na vyeti bila kuwa ujuzi haisaidii. Vyuo vinafundisha kama biashara havifundishi kuwasaidia ujuzi wa maisha... tunaamini kwamba Tanzania kuna nafasi za ajira kwa kampuni nyingi binafsi lakini watu wanasoma kozi ambazo hazina ajira," amesema.
Amefafanua kuwa, fursa zipo nyingi isipokuwa watu wengi wanashindwa kutumia fursa na kuilaumu Serikali.