šAipongeza REA kwa kufikisha umeme vijijini
šAsisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia
šApokea taarifa ya miradi ya REA inayoendelea
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakati akifunga Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024 uliofanyika leo tarehe 5 Disemba, 2024 jijini Arusha.