MKURUGENZI WA INEC APIGA KURA KATIKA KITUO CHA MAKOLE JIJINI DODOMA

 


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amepiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Chadulu kilichopo Kata ya Makole katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma asubuhi ya leo tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo nchini.

Akizungumza baada ya kupiga kura Bw.Kailima amewaasa wananchi wajitokeze kupiga kura kuwachagua wanyeviti wa serikali ya mtaa, kijiji au kitingoji, wajumbe wanawake na wajumbe mchanganyiko katika maeneo yao.

Amesema zoezi la kupiga kura halichukui muda mrefu kwani ndani ya dakika mbili unakamilisha haki ya kikatiba kuchagua viongozi katika uchaguzi huo.

Hivyo, amewasihi watanzania wote kwa ujumla na wapiga kura wa mtaa wa Chimuli II kufika kwenye vituo vya kupigia kura na kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika leo nchini baada ya wiki moja ya kampeni za uchaguzi na vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa 2.00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.


Post a Comment

Previous Post Next Post