Mawakala Forodha Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Weledi, Waaswa Kujiepusha Na Vitendo Vya Rushwa









Na Mwandishi wetu.
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amewataka mawakala wa forodha nchini kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mwenda amesema hayo, leo Julai Mosi, 2024 alipokutana na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) wakiongozwa na Rais wa Chama hicho, Edward Urio kwa lengo la kusikiliza changamoto zao, kujadiliana namna ya kuzitatua na kuboresha huduma za forodha ili kuhakisha wanalipa kodi stahiki na kwa hiyari

Kikao hicho kimefanyikia katika ukumbi wa mikutano wa TPA, jijini Dar es Salaam.

Aidha kamisha amewahakikishia wanachama hao kuwa ameyachukua maoni yao na changamoto kwa yale yaliyokuwemo ndani ya uwezo wao watakwenda kuyafanyia kazi na yale ya kisera watayapeleka sehemu husika

Naye, Rais wa TAFFA, Edward Urio amesema kuwa ushirikiano wao na maofisa wa idara ya forodha umeifanya idara hiyo kuvuka malengo walioyowekewa katika ukusanyaji kodi kwa mwaka fedha 2023/2024.

"Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia idara ya forodha walivuka malengo ya ukusanyaji wa kodi kutoka na ushirikiano mzuri wa kati ya maofisa wa TRA na sisi mawakala wa forodha"

"Sisi mawakala wa forodha ni sehemu ya ushirikiano na TRA kwenye kukusanya kodi kwa niaba ya serikali "

Amesema kuwa mawakala wa forodha wamefurahi kuona namna ambavyo Kamishna Mkuu wa TRA alivyoona umuhimu wao kwa kukubali kukutana nao kwa ajili ya kujadiliana namna ya kuongeza usanifu wa ukusanyaji kodi na kuboresha ushirikiano .

"Tunamhakikishia Kamishna Mkuu kuwa malengo aliyopewa si yake pakee yake tutashirikiana naye kuhakikisha yanatimia"

Post a Comment

Previous Post Next Post