Zaidi ya wakulima 6o wamefika katika vipando vya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) vilivyopo katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza kwa vitendo matumizi sahihi ya mbolea na mbinu bora za kilimo kwa ujumla. Wakulima hao wamejionea tofauti iliyopo kati mazao yaliyowekwa mbolea na yasiyowekwa hivyo kuelezwa umuhimu wa
kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao kwa kuzingatia mambo muhimu ikiwemo kutumia mbolea kwa wakati sahihi, kwa kiwango sahihi, chanzo sahihi na mahali sahihi.
Bi. Schola Mbalila,
Kaimu Meneja wa Udhibiti Ubora na Majaribio (TFRA) amekuwa akipokea wageni mbalimbali katika vipando hivyo na kutoa maelezo ya kitaalam kwa wakulima
Wakulima wakifumdishwa matumizi sahihi ya Mbolea kwa vitendo
Wakulima mbalimbali wakiwa wanapata elimu ya matumizi ya mbolea kwenye vipando vya TFRA
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma wakipata elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwenye zao la Alizeti