TFRA yapongezwa upatikanaji wa mbolea Arumeru

 Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Kaganda ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kuhakikisha mbolea ya ruzuku inapatikana katika Wilaya hiyo.

Kaganda amesema, upatikanaji wa mbolea kwa wakati unawawezesha wakulima kuhudumia mashamba yao kwa kutumia mbolea stahiki kwa wakati,  na hivyo kuongeza  uzalishaji utakaokuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla. 

Mhe. Kaganda  ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Mamlaka kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa  Mkutano wa mwaka wa wadau wa Mamlaka ya  Afya ya Mimea na Viuwatilifu Tanzania ( TPHPA) uliofanyika tarehe 21 June, 2024  katika Viunga vya ofisi ya Mamlaka hiyo  Jijini Arusha.

Kaganda ameeleza kuwa kwa sasa mbolea inapatikana na malalamiko yamepungua kwa kiasi kukubwa ukilinganisha na msimu wa kilimo uliopita.

Mkutano huo umefanyika  sambamba na Maonesho ambayo TFRA pia imeshiriki.



Post a Comment

Previous Post Next Post