NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Tume ya Madini inaendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote kutoka katika Mkoa wa Dodoma kwenye Wiki ya Maonesho ya Madini inayoambatana na Kongamano la Wachimbaji wa Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, leo tarehe 22 Juni 2024, Dodoma.
Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.
Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.