Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent mwishoni mwa wiki ametembelea kiwanda cha mbolea na uchimbaji wa madini ya PHOSPHATE Minjingu ili kujionea hali ya uzalishaji kiwandani hapo.
Pamoja na kujionea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi, Laurent alipokea pongezi katika usimamizi wa mbolea za ruzuku lakini pia amepokea changamoto wanazokabiliana nazo wazalishaji wa mbolea.
Aidha, amewataka kuwasilisha maoni yao ya namna ya kuboresha tasnia ya mbolea ili kwa pamoja washirikiane katika kuwahudumia wakulima nchini.


