COSTECH YAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI YA TEKNOLOJIA

 Mwandishi Wetu


MTAALAMU wa Ushirikiano kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Promise Mwakale amesema wanavyozidi kwenda mbele ndiyo wanavyozidi kuelewa jinsi tume itakavyoweza kusaidia miradi ya teknolojia.

Mwakale amesema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa naCostech ili kuajadiliana na kuangalia jinsi gani teknolojia inavyoweza kulindwa kabla haijapelekwa katika jamii, ikiwa ni sehemu moja wapo ya maadhimisho ya wiki ya Ubunifu.

"Kwa jinsi tulivyoanza kutoka kusaidia teknolojia ya za kawaida, kwa sasa hivi tunaweza kutengeneza bunifu mbali mbali na teknolojia ambazo zina bunifu yaani tumeongeza thamani,"

Amesema, kuna kitu tofauti ambacho wataalam wetu kwa kushirikiana na wabunifu wametengeneza hivyo wanavyozidi kwenda mbele ndipo teknolojia yenye thamani zaidi inazidi kutengenezeka.

Ameongeza kuwa,  kwa kushirikiana na chuo kilichopo nje ya nchi (Greenwich) wameweza kusaidia Teknolojia ya zao la muhogo ambayo ineweza kuwekwa kwenye sehemu yoyote ili mradi kuwepo na mita 25 za muhogo.

Aidha Mwakale amesema pia wameshirikiana na Chuo cha Sokoine kutengeneza unga lishe ambao hauna sumu kuvu, ambapo chuo hicho kimeweza kusaidia teknolojia na fomula ambayo imetumika kutengeneza unga huo.

"Tumeweza pia kushirikiana na Chuo cha Nelson Mandela ambacho kina teknolojia inayosaidia wabunifu wa ngozi kutengeneza ngozi ambayo itatumia magamba  yanayopatikana hapa nchini...., Hii inaonesha kwamba vyuo vinaweza kushirikiana na wajasiliamali kutengeneza teknolojia ambazo zina manufaa kwetu na kuweza kutatua matatizo yetu katika jamii," alisema Mwakale

Naye Kiko Kiwanga, mmoja wa washiriki wa washa hiyo kutoka mkoani Morogoro, amesema wameajadiliana kwa upana na  kuangalia ni jinsi gani teknolojia inaweza kulindwa kabla haijapelekwa katika jamii na kuweza kutumika kwa sababu usipo fanya hivyo hautaweza tena kuilinda na manufaa yanaweza kuwa madogo sana katika jamii kwa sababu kutakuwa hamna manufaa ya kutosha kwa wale ambao wamejihusisha kutengeza  teknolojia hiyo na kuhakikisha kwamba inakuwepo," amesema Kiwanga

"Kuna mambo mengi ambayo nimejifunza, tupo kwenye teknoloji muda mrefu ila kuna vitu vipya tumejifunza tumeweza kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali kutoka Brela, vyuoni, ambao wameweza kutueleza vitu ambavyo tunaweza kufanya hasa katika hizi teknolojia namna ya kuzilinda kabla hazijawafikia walaji,"amesema.


Mtaalam wa Mashirikiano kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Promise Mwakale akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ili kuajadiliana na kuangalia jinsi gani teknolojia inavyoweza kulindwa kabla haijapelekwa katika jamii, ikiwa ni sehemu moja wapo ya maadhimisho ya wiki ya Ubunifu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Intermech Engineering Limited Mhandisi Peter Chisawillo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Costechi jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post