Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inashiriki katika maonesho ya wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Maonesho hayo ya siku tatu yanayofanyika katika Shule ya Uhandisi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Dar e Salaam, yanahusisha tafiti na bunifu mbalimbali ambazo zimefanywa na wavumbuzi.
Akitoa mchango wake katika Semina ya Wahadhiri na Wanafunzi wa Fani za Teknolojia, Afisa Mwandamizi kutoka BRELA Bw. Raphael Mtalima amewashuri kuhakikisha kuwa bunifu mbalimbali zinazofanyika haziishii katika nadharia bali zisajiliwe na kuingizwa katika mchakato rasmi ili Utafiti na Ubunifu uzidi kukua kwa Ustawi wa uchumi wa Tanzania.
Bw. Mtalima amewahimiza pia watafiti wanaotarajia kuingiza bidhaa au bunifu zao sokoni kuzisajili BRELA kupitia huduma ya usajili kwa njia ya mtandao.
BRELA itaendelea kutoa mafunzo na kuwafikia wabunifu mbalimbali katika maonesho hayo yatakayo hitimishwa April 14, 2023.