Naibu Katibu Mkuu Mpya Maliasili Apokewa

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amewaongoza menejimenti na wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Katibu Mkuu mpya Bw. Anderson Mutatembwa aliyeapishwa jana Ikulu.

Aidha, leo pia ofisi za Wizara hiyo Mtumba Dodoma, Dkt. Abbasi amewaongoza wafanyakazi hao kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Bw. Juma Selemani Mkomi aliyeapishwa jana kuwa Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Utumishi.

“Leo tunapokutana hapa kumuaga Bw. Mkomi na kumkaribisha Bw. Muta labda mfahamu tu sisi watatu hapa tunafahamiana siku nyingi na kubwa wote tulikuwa katika Timu iliyoratibu kwa mafanikio makubwa ushiriki wa Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Tour na sote tulizunguka naye Mhe Rais nchi nzima kwa hiyo tunaufahamu mkubwa wa jinsi ya kuutangaza utalii kwa kiwango kikubwa,” alisema Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Mkomi amewashukuru wafanyakazi hao kwa ushirikiano mkubwa waliompa akiwa Wizarani hapo huku Bw. Muta naye akiahidi kujifunza haraka ili kazi iendelee na kuomba ushirikiano wa wafanyakazi wote.



Post a Comment

Previous Post Next Post