TANESCO WATOA MATUMAINI KWA WANANCHI UPUNGUFU WA UMEME KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI

 


Shirika la Umeme Nchini( TANESCO) limesema kuwa upungufu wa Umeme uliopo  kwa sasa ni kiwango cha Megawati 300 hadi 350 hali ambayo imechangia kuwepo kwa ukosefu wa umeme kwenye maeneo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu Tanesco *Mhandisi Maharage Chande* amesema kwamba kufuatilia hali hiyo shirika hilo limechukua jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha upungufu wa umeme unapunguza.

Alisema kuwa sababu kubwa zilizosababisha upungufu huo ni pamoja na hali ya  ukame mkubwa inayoendelea nchini ambao umesababisha kituo cha kuzalisha umeme cha  Kihansi ,Pangani na Mtera kupungua maji nakupungua kwa uzalishaji wa umeme kwenye vituo hivyo.

Aidha alisema pia kuwa sababu   nyingine ni matengenezo ya mitambo  yanayoendelea kwa sasa ambapo yanafanyika matengenezo kinga na matengenezo makubwa akitolea mfano kituo cha gesi cha  Ubungo iii ,pamoja na kituo cha kidatu.

Hata hivyo amesema kuwa mwezi Desemba na Januari matumizi ya umeme huongezeka katika  baadhi ya mikoa akitolea mfano Dar es salaam na Pwani kutokana na mikoa hiyo kuwa katika kipindi cha joto nakutumia umeme mwingi kwa matumizi ya vifaa vya umeme kama vile feni na Koyoyozi.

Aidha amesema kuwa katika mipango ya muda mrefu ni kukamilisha ujenzi wa bwawa la nyerere ambapo ujenzi huo mpaka sasa ni asilimia 77 ambapo ujenzi huo ukikamilika utasaidi kupunguza changamo kubwa ya umeme inayojitokeza kutokana na sababu za kupungua kwa kina cha maji kwenye mabwawa ya Mtera, Kihansi na Pangani.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa umeme kwa  kutumia gesi ya Mtwara *Mhandisi Chande* amesema kwamba gesi ya Mtwara tayari imeanza kutumika na hadi sasa ni asilimia 75 ya gesi hiyo inatumika kuzalisha umeme.

Aidha amesisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kutoa taarifa ya hali ya umeme mara mbili kwa wiki yaani siku ya Jumatatu na Ijumaa ili kuwezesha wananchi kufahamu uhalisia wa hali ya upungufu wa Umeme iliyopo nakusaidia kuepukana na upotoshaji unaotolewa na baadhi ya watu kuhusu hali hiyo

Post a Comment

Previous Post Next Post