Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akifungua
mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo makamishna/wajumbe wapya na
maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi
Wanachama wa SADC (ECF-SADC). Mafunzo hayo yanahusisha wajumbe wapya wa
Tume za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la
ECF-SADC ambazo ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia,
Zimbabwe, Lethoto, Malawi na Tanzania na yameanza leo Novemba 22 hadi 25
,2022 jijini Dar es Salaam.
Mwekiti
wa Jukwaa la ECF-SADC ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Namibia, Elsie Nghikembua akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo wajumbe wapya wa Tume za Uchaguzi
na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambazo ni
Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lethoto,
Malawi na Tanzania wanashiriki mafunzo hayo ya siku nne.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mabruki Makame
akizungumza nebo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam
leo Novemba 22,2022.
Mgeni
rasmi wa ufunguzi wa mafunzo kwaajili ya Makamishna /Wajumbe na Maofisa
waandamizi kutoka Tume za Taifa za kutoka nchi wanachama wa ECF-SADC,
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele
(katikati) wakiwa katika ufunguzi huo leo jijini Dar es Salaamz. Kushoto
ni Mwekiti wa Jukwaa la ECF-SADC ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Namibia, Elsie Nghikembua na Kulia ni Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera Charles.
Makamishna/Wajumbe
na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za
Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo
hayo.
Olufunto Akinduro akiendesha mjadala wakati wa mafunzo hayo.
Harris Patani akiongoza mijadala wakati wa mafunzo hayo.
Makamishna/Wajumbe
na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za
Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo
hayo.
Picha za pamoja za viongozi na washiriki
****
Jukwaa
la Tume za Uchaguzi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini
mwa Afrika (ECF – SADC) kwa kushirikiana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) na Taasisi ya International IDEA wameandaa mafunzo ya siku nne ya
kuwajengea uwezo Makamishna wapya na maafisa waandamizi wa Tume ambazo
ni wanachama wake.
Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 22,2022 jijini Dar es Salaam yanataraji kufikia tamati Novemba 25, mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema nchi 9 wanachama wa
Jukwaa la ECF-SADC ambao ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botwana,
Namibia, Zimbabwe, Lesotho, Malawi na Tanzania wanashiriki mafunzo hayo.
Aidha Jaji Mwambegele amesema baadhi ya nchi ikiwemo Afrika
kusini zitashiriki katika mafunzo haya kwa njia ya mtandao (Virtually).
Amesema
wajumbe na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi watapata fursa ya
kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika kuboresha
utekelezaji wa majukumu yao.
“Washiriki watajifunza na
kubadilishana uzoefu wa namna ambayo uchaguzi umekuwa ukifanyika katika
nchi zao na kuona changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na namna ya
kuzitatua,”alisema Jaji Mwambegele.
Aidha Jaji Rufaa Mwambegele
amezitaja mada zitakazowasilishwa katika mafunzo hayo kua ni pamoja na
demokrasia, uchaguzi na menejimenti ya uchaguzi; Vigezo vya kimataifa
vya upimaji wa uchaguzi na wajibu wa kuendesha chaguzi za kidemokrasia;
Usimamizi wa uchaguzi: Tafsiri, mifano, majukumu na na nguvu ya
kisheria.
Mada nyingine amezitaja kuwa ni pamoja na Mifumo ya
uchaguzi, Mzunguko wa uchaguzi, kalenda ya uchaguzi na mipango ya
uchaguzi, Matumizi ya TEHAMA katika chaguzi, Masuala
yanayojitokeza katika usuluhishi wa migogoro ya uchaguzi na utoaji haki
za katika uchaguzi na Uandikishaji wa wapiga kura.
Pia zipo mada
za siku ya uchaguzi (kupiga kura) na menejimenti ya matokeo, Changamoto
kwa Tume za Uchaguzi, Uongozi wa Tume za Uchaguzi, utendaji kazi na
uendelevu wake, Ushawishi kwa Wadau wa uchaguzi, changamoto na uhusiano
na Tume; Kuendesha Uchaguzi Jumuishi kwa kuzingatia jinsia, vijana na
watu wenye ulemavu.
Jaji Rufaa Mwambegele amezitaja mada zingine
kuwa ni pamona na Menejimenti ya mashinikizo ya kisiasa;, Kugharamia
uchaguzi na Tume za uchaguzi ; Ushirikiano kati ya Tume za uchaguzi na
vyombo vya habari na mawasiliano ya nje ya taasisi pamoja na masuala
yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano ya kidigitali.
Mada
za Kukabiliana na majanga na kujenga uwezo wa namna ya kukabiliana na
changamoto zinazoweza kujitokeza na Usalama wakati wa uchaguzi, vurugu
na namna ya kutatua changamoto pia zitatolewa.
“Baada ya kupatiwa
mafunzo ni matarajio kuwa watendaji hawa watakwenda kuhakikisha kuwa
chaguzi zinakuwa huru, za haki na zenye kuaminika. Hii itasaidia katika
kukuza demokrasia itakayochochea amani, usalama na ustawi wa wananchi na
Taifa,”alisema Jaji Rufaa Mwambegele.