Naibu Katibu Mkuu Wizara Ya Maji Atembelea Mradi Mkubwa Wa Maji Longido

 Na Jane Edward, Arusha


Naibu Katibu mkuu wizara ya maji ,Mhandisi Nadhifa Kemikimba ametembelea mradi wa maji wilayani Longido na kusema wameridhishwa na mradi huo unavyotekelezwa.

Aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wilayani Longido unaotekelezwa na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA)huku akifuatana na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo ya Afrika katika kujionea miradi hiyo ilipofikia na maendeleo yake.

"Kwa kweli tumefurahishwa Sana na ugeni wa Mkurugenzi mtendaji wa benki hi ambao wameweza kuridhishwa na matumizi ya fedha tulizotumia katika mradi huu, na kuwa fedha tulizopewa hatujazifanyia mchezo na hakuna mahali tumechelewesha tangu kuanza kwa mradi huu."alisema .

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya maendeleo ya Afrika ,Amos Cheptoo ameeleza kuridhishwa na serikali ya Tanzania katika usimamizi wa matumizi ya fedha hizo zilizotolewa na benki hiyo kutekeleza mradi mkubwa wa maji jijini la Arusha na maeneo jirani .

"Naipongeza sana serikali kupitia wizara ya maji pamoja na AUWSA kwa namna ambavyo wameweza kuwekeza katika.sekta ya maji kwa kutekeleza mradi huo kwa umakini na uaminifu mkubwa ambapo mradi huo ukikamilika utaweza kuwanufaisha wananchi wengi na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji na hatimaye kuweza kupunguza maradhi yatokanayo na ukosefu wa maji kwa ujumla."alisema.

Naye Mkurugenzi wa AUWSA jiji la Arusha,Mhandisi Justine Rujomba alisema kuwa,hivi Sasa wameshakamilisha zoezi la mfumo wa majitaka na kinachofanyika Sasa hivi ni ulazaji wa mabomba ya maji Safi na kuwa mradi huo umeweza kupunguza makali ya mgao wa maji .

Mhandisi Rujomba alisema kuwa,hapo awali walikuwa wanapata kiwango cha maji Lita milioni 40 kwa siku ambapo kwa Sasa hivi wanapata kiwango cha lita milioni 60 kwa siku ,hivyo kuondoa kabisa changamoto ya mgao wa maji .



Post a Comment

Previous Post Next Post