Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Balozi Elisabeth Jacobsen wakati alipokuwa na kikao na balozi huyo katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam, Novemba 16, 2021.
Waziri wa Nishati, January Makamba (katikati), wakiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Balozi Elisabeth Jacobsen (tatu-kushoto) Naibu Balozi wa Norway, Bjorn Midthun (pili-kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Seif Saidy (pili-kushoto) Mshauri Nishati wa Ubalozi wa Norway, Morten Heide(kwanza-kulia) mara baada ya kumaliza kikao na balozi wa Norway, kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam, Novemba 16, 2021.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Balozi Anders Sjoberg wakati alipokuwa na kikao na balozi huyo katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam, Novemba 16, 2021.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akizungumza na Kaimu Balozi wa Saud Arabia nchini Tanzania, Fahd Al-harbi wakati alipokuwa na kikao na balozi huyo katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam, Novemba 16, 2021.
Picha mbalimbali wakati Waziri wa Nishati, January Makamba alipokutana na kufanya kikao na mabalozi wa Norway, Sweden na Saud Arabia, katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam. Novemba 16, 2021.
*****************************
Hafsa Omar-Dar es Saalam
Waziri wa Nishati, January Makamba amezishukuru nchi za Norway, Sweden na Saud Arabia kwa mchango mkubwa unayoipatia Tanzania katika kuendeleza sekta ya Nishati.
Ameyasema hayo, Novemba 16, 2021 kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa na kikao na mabalozi wa Norway, Sweden na Saud Arabia, katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam.
Akizungumza na mabalozi hao, amesema nchi hizo zimeendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania kwa kufadhili miradi mbali mbali katika Sekta ya Nishati.
Alieleza kuwa, Serikali itaendelea kunufaika na fursa mbalimbali zinazotelewa na nchi hizo kwakuwa nchi hizo zipo tayari wakati wowote kufanya kazi na Serikali ya Tanzania.
Aidha, amewataka mabalozi hao kuendelea kutoa ushirikiano katika kuendeleza sekta ya nishati ambayo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania.
Kwa upande wake, Balozi wa Norway, Balozi Elisabeth Jacobsen amesema Tanzania ni nchi ambayo inajulikana kwa historia yake ya kuwa na mashirikiano mazuri kwa mataifa mengine.
Ambapo ameeleza kuwa uhusiano baina ya nchi mbili hizi umedumu kwa takribani miaka 50 ambapo kwa kuzingatia ushirikiano huo nchi hiyo imefadhili miradi mbalimbali katika sekta Nishati na itaendelea kufadhili katika miradi mbalimbali katika sekta hiyo.
Nae, Balozi wa Sweden, Balozi Anders Sjoberg, ameeleza kuwa nchi yake inajivunia kuwa sehemu ya maendeleo katika sekta ya Nishati nchini Tanzania, ambapo alieleza kuwa nchi yao imefadhili miradi ya mbalimbali ya umeme kama mradi wa Umeme vijijini, Ujazilizi na miradi mengine ya umeme ambayo muhimu na inawanufaisha watanzania wote kwa ujumla.
kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Saud Arabia, Fahd Al-harbi, alisema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza sekta ya nishati nchini kwa muda wowote kwakuwa sekta hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi