WAZIRI JAFO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUWA NA MFUMO BORA WA MAJITAKA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua mfumo wa majitaka katika mabwawa yanayotibu majitaka kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma leo Mei 7, 2021. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph na wa tatua kulia ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin Rwezimula.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiangalia mojawapo ya chemba za kupokea majitaka alipofanya ziara katika mabwawa yanayotibu majitaka kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma leo Mei 7, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiangalia mojawapo ya chemba za kupokea majitaka alipofanya ziara katika mabwawa yanayotibu majitaka kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma leo Mei 7, 2021. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph.

*************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo amezitaka mamlaka za maji nchini kuwa na mifumo bora ya majitaka ili kuyadhibiti yasitiririke ovyo na kuhatarisha mazingira na afya.

Jafo ametoa agizo hilo leo Mei 7, 2021 alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa agizo alilolitoa alipotembelea eneo hilo hivi karibuni na kutoridhishwa na usimamizi wa majitaka katika mabwawa yanayotumika kutibu majitaka kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Pia alikemea tabia ya baadhi ya watu kutupa taka ngumu katika mifumo ya majitaka hali inaweza kusababisha mifumo hiyo kuziba na hivyo majitaka hayo kushindwa kudhibitiwa.

“Ninyi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kaeni na wenzenu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuna changamoto ya uchafu hapa tunaona solid waste (taka ngumu) zinatupwa hapa na waambieni watu wao wa usafi wasitupe hizi barakoa, zinaziba na zinaweza kuhatarisha afya zikiinghia katika mazingira,” alisema.

Aidha, Jafo aliipongeza mamlaka hiyo kwa kufanyia kazi agizo lake la kuondoa uchafu ulioziba katika chemba hali ambayo ingeweza kusababisha uchafu huo kusukumwa na mvua na kutiritrika kwenye vyanzo vya maji.

“Mkurugenzi naomba nikupongeze unakumbuka nilikuja hapa nikakuta uchafu hata mfereji ulikuwa hauonekani ndio maana nikatoa wiki moja sasa nimekuja na nimemekuta mazingira mazuri,” alisema.

Hata hivyo, aliitaka DUWASA kutoa elimu kwa wananchi wa Dodoma kuhusu matumizi ya mifumo ya majitaka ikiwemo kuacha kutupa taka ngumu katika mifumo hiyo.

Katika hatua nyingine waziri huyo alitoa wito kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuyatumia mabwawa ya majitaka yaliyopo katika eneo hilo kama sehemu ya kufundishia wanafunzi wanaochukua masomo ya mazingira.

Waziri Jafo alisema kuwa hatua ya kuwapeleka katika maeneo hayo wanafunzi hao kwa ajili ya kusoma kwa vitendo itawajengea uelewa zaidi kuhusu masuala ya mazingira.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph alisema kuwa wataendelea kuyatunza mabwawa hayo ili yaendelee kuhifadhi mazingira.

Alimshukuru Waziri Jafo kwa kufanya ziara za mara kwa mara kukagua mifumo ya majitaka inayosimamiwa na DUWASA na kutoa maelekezo mbalimbali kwa lengo la kubotresha mazingira.

Mhandisi Joseph alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvuja kwa majitaka katika mitaa ya jiji hilo kutokana na matumizi yasiyofaa kinyume na ilivyokusudiwa.Naye Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin Rwezimula alisema jukumu la kuhakikisha majitaka yanadhibitiwa ni la mamlaka za maji.

Alisema kuwa NEMC inafanya kaguzi za mara kwa mara na endapo inabaini changhamoto inamtaka mhusika arekebishe mara moja ili kulinda mazingira na afya za wananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post