Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akibadilisha fimbo kutoka kwa
Freddy Lukala ili kuweza kuupiga mpira kwenye muelekeo unaofaa wakati
akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana
uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameshika fimbo kuupiga
mpira wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu
wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia
michezo
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameupiga mpira wakati
akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana
uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na mchezaji
mwenzake Dkt. Aloyce Subhamilia na mara baada ya kufanya mazoezi
mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani
Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo.
***************************
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wizara yake imeanza
juhudi za kufungamanisha michezo na Utalii kwa maana ya Utalii wa
Michezo ikiwemo ya Soka na Gofu
Amebainisha hayo
mwishoni mwa wiki wakati akifanya mazoezi ya gofu katik Uwanja
Gymkhana Gofu Klabu uliopo mkoani Morogoro aliyoyafanya kwa muda wa siku
nne asubuhi na jiono kwa lengo la kukuza utalii kupitia mchezo wa
Gofu.
Hatua hiyo ya
uhamasishaji ya kufanya mazoezi ya Gofu, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt.Damas Ndumbaro amefanya wakati wa akifanya mikutano na Wadau wa
Utalii iliyofanyika kwa muda wa siku nne mfululizo mkoani hapo.
Amesema Wizara imejipanga kuhakikisha
inaufanya mchezo wa Gofu kuwa kichochea cha kukuza utalii kwa kuandaa
mashindano yatakayo wakutanisha watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya
nchi.
Akizungumzia
mikakati ya kukuza utalii wa michezo, Waziri Ndumbaro amesema ameiagiza
Menejimenti ya Hifadhi ya Mikumi kuukarabati uwanja wa mpira wa miguu
uliopo katikati ya Hifadhi hiyo ili timu mbalimbali ziweze kuutumia
uwanja huo kwa ajili ya mechi pamoja na kufanyia mazoezi ikiwemo timu ya
Simba na Yanga.
Amesema
kuukarabatiwa kwa uwanja huo kutasaidia kuongeza idadi ya Watalii
wanaotembelea Hifadhi hiyo ambapo amesema watu mbalimbali wakiwemo
wachezaji na Mashabiki watakwenda kuangalia mechi wakat huo huo
watapata fursa ya kuangalia makundi mbalimbali ya Wanyamapori wakiwa
mbali kidogo ya uwanja wakiwemo nyati, simba pamoja twiga
Amesema katika
nyakati za jioni Wanyamapori hao hupendelea kula chakula karibu na
Uwanja huo, hivyo watazamaji wataweza kuufaidia
Amesema mbali na
uwepo wa uwanja wa mpira wa miguu katika Hifadhi hiyo kuagiza
ukarabatiwe, Pia ameagiza litafutwe eneo lingine katika Hifadhi kwa
ajili ya kutengeneza uwanja wa kikapu hatua itayosaidia kuwavuta
Mashabiki na Wachezaji wa mpira wa miguu kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi.
Pia, Waziri
Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na
Wadau mbalimbali inatarajia kufanya mashindano makubwa katika uwanja wa
Gofu wa TPC Moshi kwa yatakayowakutanisha Wachezaji wakubwa wa mchezo
huo wa kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuitangazia Dunia kuwa
Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na ni sehemu pekee utakayoweza kuupanda
Mlima huu na sio kwingineko.
Katika hatua
nyingine, Dkt.Ndumbaro ameipongeza Klabu ya Simba kwa uamuzi wa kuwa
Wazalendo kwa kuitumia nembo ya “Visit Tanzania” katika kutangaza
vivutio vya utalii vilivyopo nchini.