VIONGOZI WA MICHEZO NIRC KUITANGAZA TUME KUPITIA SEKTA MICHEZO

 

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi Mary Mwangisa akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu Dodoma wakati wa Uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Michezo katika Taasisi hiyo.
Mawakala wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura baada ya Uchaguzi huo.
Bw. Danny Makange Msanifu Kilimo ambaye ni  Katibu wa Baraza la michezo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumzia mipango mikakati ya baraza hilo jipya
Bw. Godwin Mutahangwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akizungumza kama Msimamizi wa Uchaguzi wa Baraza la Michezo la Ofisi hiyo wakati wa uchaguzi uliofanyika jana jioni katika viunga vya ofisi hiyo jana jioni.
Picha ya Pamoja Ikionesha baadhi ya Viongozi wa Baraza la Michezo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika katika ofisi hizo Makao Makuu ya nchi Dodoma jana jioni, kutoka kushoto ni Bi Fatma Mwera Afisa Kilimo wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni katibu msaidizi,katikati, Bw. Yassin Kazoba Mchumi, Mwenyekiti wa Baraza la michezo na Bi Nyandaro Mapesi mtunza kumbukumbu ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo.

                             Na MwandishiWetu Dodoma

Viongozi wa Baraza la Michezo wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliochaguliwa katika kinyanganyiro kikali cha kugombea nafasi za Mwenyekiti na Mwenyekiti Msaidizi wa Michezo, pamoja na nafasi ya Katibu mkuu na Katibu mkuu msaidizi, wameapa kukuza tasnia ya michezo katika Taasisi hiyo nakutumia fursa walioipata kutangaza shughuli za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia sekta ya Michezo.

Akizungumza baada ya uchaguzi huyo Mwenyekiti aliyeshinda Bw. Yassin Kazoba Ambaye ni mchumi, ametoa ahadi yakushirikisha watumishi wote wa Tume katika shughuli za michezo kwani Utendaji wa kazi unategemea afya za watumishi.

Katibu wa Baraza hilo jipya Bw. Danny Makange alisema anamkakati wakuainisha wachezaji katik a Ofisi za Tume nchi nzima ilikuweza kupata ushindani katika michezo ya mabonanza na mashindano mengine na mashirika naTaasisi za Serikali.

Pia kuunganisha wanamichezo na wadau ilikuwezesha taasisi na shughuli zake zifahamike.

Kwaupande wake Mkurugenziwa Utawala na Rasilimali watu Bi, MARY MWANGISA amewataka viongozi hao pamoja na kutekeleza wajibu katika shughuli za michezo, waongeze bidii ya kazi ili Taasisi hiyo iweze kufikia malengo ya kimkakati la kukuza eneo la Umwagiliaji zaidi la Hekta zaidi laki sita zinazomwagiliwa kwasasa,kufikia Hekta Milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka 2025.

Awali Mwenyekiti wa uchaguzi huoBwGodwin Mutahangarwa ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha sheria, amewataka viongozi hao kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kuushukuru uongozi wa Taasisi kwa kuunda chombo hicho ambacho ni muhimu sana na namna mojawapo yakuwashirikisha wafanyazaki na kujenga uhusiono mwema kati ya wafanyakazi na Taasisi naTaasisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post