baadhi ya wakulima wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Nakahuga wakifuatilia mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mkulima katika skimu ya kilimo cha uwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho wilayani Songea Bw. Albert Mtani akiuliza swali wakati wa mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Na Mwandishiwetu – Peramiho
Wakulima katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma wameipokea sheria ya Taifa ya kilimo cha umwagiliaji na kuonesha utayari wa kuchangia katika mfuko wa maendeleo yakilimo cha umwagiliaji kwa kukiri kuilewa sheria hiyo mara baada ya mafunzo waliyopata toka kwa wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Akizungumza wakati wa mkutano wa majumuisho uliofanyika katika kijiji cha Nakahuga,mmoja wa wakulima hao Bw. Albert Mtani alisema kuwa kilimo cha umwagiliaji kwao ni mkombozi kwani ni kilimo cha uhakika.
“Binafsi ninaishukuru serikali kwa kuleta mradi huu nani naamini inania njema ya kuendelea kuboresha miondombinu katika skimu hii na kwa kuwa tunapata faida nyingi zitokanazo na shughuli zetu zakilimo, hivyo sio ni tatizo kwenye uchangiaji katika mfuko kwani ninaamini kuwa mifereji itakapo haribika kwa namna yoyote ile serikali itaitengeneza kupitia mfuko huo, na tutaendelea na shughuli zetu za kilimo bila wasiwasi.” Alisema.
Sambambana hilo kwa nyakati tofauti katika ushiriki wa mkutano huo, baadhiya wakulima walisikika wakisema kuwa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji sasa imekaa vizuri kwani kabla yakuwepo kwa sheria hiyo ushirikishwaji wa wakulima kuhusu shughuli za umwagiliaji ulikuwa ni mdogo na kulikuwa na usimamizi mbovu wa miundombinu yaumwagiliaji
Waliongeza kwa kusema kuwa sheria ya Taifa ya umwagiliaji pia itaweza kusaidia kutatua migogoro midogo midogo iliyopo katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.