KATIBU MKUU DK.ALOYCE NZUKI AWAPONGEZA SAO HILL KUVUKA LENGO LA UKUSANYAJI WA MAPATO

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

 

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.

 

Katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na
Utalii amewapongeza TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill lililopo wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa kwa kuvuka lengo la makusanya ya mapato ya mwaka.

 

Akizungu alipokuwa alipotembelea Shamba
la Miti Sao Hill,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki alisema
kuwa ameona shughuli za upandaji miti za utunzaji  zinazofanywa na shamba
.

 

Alisema kuwa anatoa pongezi hizo kwa
TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwa kufaya kazi nzuri ambayo hupelekea
taifa kunufaika kutokana na uwepo wa Shamba hili ambalo ni shamba kongwe na
shamba kubwa kuliko mashamba yote ya miti ya kupandwa nchini.

 

“Mnafanya kazi nzuri
sana,nimeona hapa kwenye taarifa yenu ,wakati wengine wamepata shida sana
kipindi cha Covid lakini ninyi mmeweza kufanya biashara vizuri, nikiangalia
jedwali ambalo Mhifadhi Mkuu amelisoma jedwali namba  tatu,naona hapa kwa
ujumla miaka hiyo mitano iliyotajwa mmevuka lengo kwa asilimia kumi na mbili
(12%) ambayo ni mafanikio mazuri sana”Alisema Dr. Aloyce Nzuki

 

“Lakini kwa mwaka ule 2018/2019
tayari mlikuwa mmeshavuka lengo kwa asilimia 28.7 (28.7) mlikuwa mko juu ya
mapato yale ya nyuma yake,na mmeonesha mnauwezo mkubwa sana wa kufanya biashara
yote inayohusiana na mazao ya misitu lakini pia ya mazao ya nyuki”,Alisema
Dr Nzuki

Aliendelea kusema kuwa kwa jitihada
hizo TFS inastahili kupongezwa na kuwataka kuendelea  kuhamasishana
watumishi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza pato la taifa.

 

Aliwaeleza watumishi kuwa utekelezaji
wa Ilani unategemea sana jitihada za watumishi walio na weredi,kujituma na
uzalendo na hivyo eneo ambalo TFS inalisimamia ni maeneo ambayo yameelekezwa na
viongozi ili kuchangia ukuaji wa pato la taifa.

 

“Niseme kitu kimoja majukumu
ambayo yapo mbele yetu  ni kutokana na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba
eneo hili ambalo mnalisimamia ambalo linatokana mazao ya misitu na nyuki ni
maeneo ambayo yametajwa na yameelekezwa na ilani yanayotarajiwa kuchangia kwa
kiasi kikubwa katika maendeleo ya taifa na mwananchi mmojammoja,”Dr Nzuki

 

Hata hivyo aliitaka TFS kupitia
Shamba la Miti Sao Hill kuendelea kuweka ushirikiano mkubwa na jamii
inayolizunguka shamba ili kuepuka majanga ambayo yanahatarisha usalama wa
shamba na mali zilizomo ambayo yamekuwa yakijitokeza

Post a Comment

Previous Post Next Post