Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akilakiwa wakati alipowasili wilayani Chemba kusikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji. |
Waziri Mpina akiwa katika kikao na Viongozi wa Wilaya ya Chemba na wataalam kabla ya kuanza mkutano wa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kidoka kusililiza changamoto za wafugaji na kuzifanyia kazi. |
Wananchi wa Kijiji cha Kidoka wakulima na wafugaji wakimsikiliza Waziri
Mpina hayupo katika picha baada ya kuwasilisha Changamoto zao
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Kijiji cha
Kidoka wilayani Chemba Mkoani Dodoma kutoa taarifa kwa wakati zinazohusu
migogoro ya wakulima na wafugaji ili Wizara yake iweze kuifanyia kazi.
Waziri
Mpina aliyasema hayo alipotembelea kijiji hicho akiwa na lengo la
kusikiliza changamoto za wafugaji ili ziweze kufanyiwa kazi ambapo
changamoto nyingi zilizotajwa na wafugaji hao zinahusisha wizara
mbalimbali ikiwa ni Pamoja naWizara ya Nishati,Ardhi na Kilimo, Mifugo
na Uvuvi.
Akianisha Changamoto hizo mwananchi mfugaji wa kijiji
hicho Bw.Abuu Mikidadi amesema kijiji hicho kinakabiliana na changamoto
ya eneo la malisho ya mifugo,ambapo kulikuwa na eneo la wazi lilitengwa
kwa ajili ya malisho lakini limevamiwa na wakulima ambapo wafugaji
wakiingiza mifugo yao wanavamiwa na kupigwa.
Alisema pia
kuna changamoto ya josho la kuogeshea mifugo pamoja na pembejeo za
mifugo,Akijibu hoja hizo Waziri Mpina alisema Serikali ni moja na
inafanya kazi kwa kushirikiana,hivyo hawezi kuyakimbia matatizo hayo na
atahakikisha anafikisha ujumbe kwa Wizara nyingine.
“Tunayo
kazi ya kufanya kama Serikali kuangalia namna gani changamoto hizi
zinaweza kut atuliwa kama vile kupunguza gharama za umeme kwa
kuzungumza na Tanesco kuweza kushusha tariffs ili wakulima na wafugaji
kijijini hapo waweze kufanyakazi bila gharama yoyote na serikali
imepunguza tozo za kuogeshea mifugo naitaleta pembejeo za mifugo na
kuuzwa kwa bei elekezi” Alisisitiza.
Waziri Mpina aliendelea
kusema kuwa “Kuna haja ya kukaa na Waziri wa Kilimo, kuangalia huu mradi
wa Umwagiliaji Chemba unaolalamikiwa na wakulima na wafugaji unawezaje
kuboreshwa ili wananchi wapate faida.” Alibainisha
Mpina
alishauri viongozi wa Serikali ya kijiji na Serikali ya Wilaya wakae ili
waweze kupata suluhisho sambamba na hilo alisema, “ Nitaleta timu
inayoshugulikia migogoro toka Wizarani kwangu pamoja na wataalam waje
hapa kutafuta majawabu yasiyo na upendeleo, asidhulumiwe mtu yoyote
asinyanyaswe mtuyeyote, kila mtua pate haki yake na wataleta
pamependekezo Serikalini.”Alifafanua
Aliendelea kusema kuwa na
hakuna mfugaji anayeruhusiwa kuingiza mifugo kwenye mashamba ya watu
wengine, na kuwataka wananchi watoe taarifa kwa wakati kwa wataalam wa
kilimo na mifugo na kwa jeshi la Police.
“Hatuwezi kuwa na mfugaji anayedharau shughuli za wengine na hakuna anayeweza kuishinda Serikali.”
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Chemba Dkt.
Semistatus Mashimba alisema kufuatia changamoto ya matumizi makubwa ya
umeme wananchi waliomba serikali kwa kupitia shirika la umeme nchini
TANESCO kuwaunganisha na umeme wa Solar ambapo mapendekezo hayo
yanafanyiwa kazi yakienda sambamba na kuangalia uwezekano wa wananchi
hao kuhamishiwa katika tariff ndogo ili waweze kumudu gharama.
Kwa
upande wa kuuza mazao ya wakulima, Mkurugenzi huyo alisema serikali
hailazimishi mkulima yoyote kuuza mazao kwa mfumo wastakabadhi ghalani
bali mkulima yupo huru kupeleka mazao popote anapotaka.