Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki amemkabidhi majukumu rasmi Dkt. Robert Fyumagwa ya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania- TAWIRI.
Dkt. Robert Fyumagwa anatekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kufuatia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori-TAWIRI, Dkt.Simon Mduma kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Kupitia hatua hiyo Dkt.Fyumagwa ameanza rasmi kutekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kuanzia tarehe 17 Agosti, 2020.
Akizungumza Jijini Arusha katika Kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Dkt. Nzuki amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano Dkt. Fyumagwa katika kutekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na kuimarisha shughuli za utafiti wa Wanyamapori pamoja na kuendeleza sekta ya wanyamapori nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akizungumza na Wajumbe wa Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori katika Kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za TAWIRI, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Malasili na Utalii, Dkt.Aloyce K. Nzuki akizungumza jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori - TAWIRI ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria, Dkt.Simon Mduma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Wanyamapori Tanzania- TAWIRI Dkt Robert Fyumagwa (kulia). Kushoto ni aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Simon Mduma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania- TAWIRI